Naibu Waziri wa Katiba na sheria Mhe Ummy A. Mwalimu akikata utepe
kuashiria uzinduzi wa Mkakati wa Usajili na kutoa Vyeti vya Kuzaliwa kwa
Watoto wenye Umri Chini ya Miaka Mitano wa Mkoa wa Mwanza.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Ummy Mwalimu akihutubia Viongozi
mbalimbali wa Serikali, Vyama vya Siasa na wananchi wakati wa uzinduzi wa
Mkakati wa Usajili na kutoa Vyeti vya Kuzaliwa kwa Watoto wenye Umri chini
ya Miaka Mitano Mkoa wa Mwanza. Mkakati unalenga kusogeza huduma za
Usajili na vyeti vya kuzaliwa katika maeneo wanayoishi na huduma hiyo
kutolewa bila ya Malipo.
Naibu Waziri wa Katiba na sheria Mhe Ummy A. Mwalimu akikabidhi Cheti cha
Kuzaliwa kwa Mzazi wa mtoto Irine Leon (aliyebebwa), Bw Leonidas
Rwehumbiza wakati wa uzinduzi wa Mkakati huo.
Naibu Waziri wa Katiba na sheria Mhe Ummy A. Mwalimu akiwa katika picha
ya kumbukumbu na baadhi ya Wageni waliohudhuria uzinduzi wa Mkakati huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...