Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salama za rambirambi kwa mama Maria Nyerere na familia yake kwa kuondokewa na mmoja wa wana familia yake, Bw. John Nyerere aliyefariki Jumamosi Mei 9,2015 katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Pamoja na salamu hizi, Rais Kikwete ambaye yuko nchini Alrgeria kwa ziara ya kikazi, amefanya mawasiliano binafsi na Mama Maria na kumpa pole kwa kuondokewa na kijana wake.

“Hakuna mzazi anayependa kuondokewa na mwanae, ni kitu kigumu sana  kwa mzazi kukishuhudia , hivyo  naelewa maumivu na huzuni kubwa uliyo nayo”. Rais amemwambia Mama Maria na kumuomba akaze moyo na kumuombea Marehemu John apate pumziko la milele.

Rais Kikwete amemhakikishia Mama Maria kuwa yeye binafsi pamoja na familia yake , wapo nae katika kipindi hiki kigumu na kuwa watashirikiana wote katika msiba huu kwa hali na mali.

Rais Kikwete anatarajia kuwasili nchini leo usiku.

Imetolewa na; 

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu - Dar es Salaam.
11 Mei, 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...