Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MAJIMBO mapya
ya uchaguzi kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) mwishoni mwa Juni, ili
kuweza majimbo hayo kupata wabunge watakaowakilisha wananchi hao.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam,Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ,Kailima Ramadhani
amesema ugawaji huo utakuwa umezingatia idadi ya watu,jiografia ya eneo husika
pamoja mawasiliano na uchumi ili kuweza kuwalishwa na bunge katika maendeleo ya
jimbo.
Ramadhan amesema katika Wilaya mpya zote zinaingia
katika jimbo la uchaguzi kinachobaki ni kupata maombi ya majimbo mengine kutoka
kwa Makatibu Tawala wa Mikoa (RAC).
Amesema kuwa baada ya maombi hayo tume ya Uchaguzi
ya Taifa itapitia mipaka pamoja na kugawa kata kutokana na kata moha haiwezi
ikawa katika majimbo mawili.
“Tunachotaka ni makatibu Tawala wa Mikoa kuleta
maombi yao mapema na kuweza kuyapitia na katika mipaka pamoja na vigezo
vilivyoanishwa na NEC”amesema Ramadhan.
Kaimu Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kailima Ramadhan akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC), juu ya ugawaji wa majimbo mapya ya uchaguzi jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari hawapo pichani walipokutana leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...