Na Avila
Kakingo, Globu ya Jamii.
WAKALA wa Huduma
za Misitu Nchini (TFS),wamewataka wawekezaji
wawekeze kwenye sekta ya ufugaji nyuki ili kutoa matokeo mazuri katika sekta hiyo.
Hayo yamezungumzwa na Afisa ufugaji nyuki mkuu wa
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Mwanahamisi Mapolu wakati akizungumza na
waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya habari MAELEZO jijini Dar es
Salaam leo.
Mapolu amesema kuwa wawekezaji wajikite zaidi katika usimamiaji wa
viwanda vitakavyozalisha vifaa vya kufugia
nyuki,visigina asali na mavazi ya kujikinga
wakati wa kulina asali.
Pia
wawekezaji wajikite zaidi katika usimamiaji wa viwanda vitakavyo zalisha bidhaa zitokanazo na
nta kama mishumaa , rangi za viatu, vilainisho pamoja na vipodozi.
Mapolu amesisitiza
kuwa sera ya ufugaji nyuki nchini
inahimiza ushirikishwaji wa wananchi katika shughuri za nyuki, uhifadhi
mazingira na uzallishaji wa mazao ya nyuki yanayokidhi mahitaji ya soko.
Pia sera ya Taifa ya ufugaji nyuki nchini inasema kuwa ili
kuhakikisha kuwa kuna mfumo thabiti wa biashara ya mazao ya nyuki, udhibiti wa
ubora wa mazao hayo ukaguzi na utaimarishwa. Biashara ya mazao ya nyuki
itahimizwa kwa kuimarisha huduma za kuaminika za udhibiti wa ubora na ukaguzi wa mazao hayo.
Afisa Ufugaji Nyuki Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
(TFS)Mwanahamisi Mapolu akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika
ukumbi wa habari Maelezo jijini Dar es Salaam leo, kushoto ni Afisa
Nyuki Masoko na Leseni, Nuru Tengeza na kulia ni Afisa Ufugaji Nyuki Mkuu,Magori Nyachari.
Afisa
Nyuki Masoko na Leseni, Nuru Tengeza akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari hawapo pichani kuhusiana na Wakala wa Huduma za Misitu Nchini (TFS) katika ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam
leo,Afisa Ufugaji Nyuki Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
(TFS)Mwanahamisi Mapolu.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria
katika mkutano wa Wakala wa Huduma za Misitu Nchini (TFS), leo jijini Dar es
Salaam.Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...