Michuzi Blog inatoa pole kwa wote waliofikwa na mafa na wote waliopoteza ama kuharibikiwa na mali zao na nyumba. Tunawaombea Mungu awape moyo wa Subira na nguvu kukabiliana na majanga haya - Ameen.
Na Abdulla Ali wa Maelezo, Zanzibar                                        
Mvua za masika zinazoendelea kunyesha Visiwani Zanzibar zimesababisha hasara kubwa ikiwemo upotevu mali na mifugo, uharibifu wa miundombinu pamoja na kusababisha vifo vya watu. 
Hadi sasa watu wawili  ambao ni Nd. Juma Hamad (25) mkaazi wa Mwanakwerekwe na mtoto mmoja  mkaazi wa Kinuni anaekisiwa kuwa na miaka 8 wamepoteza maisha. Wote wawili ni kutoka Wilaya ya Magharibi Unguja.
Hayo yamweelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud Mohamed wakati akitoa taarifa kwa wananchi kuhusiana na athari za mvua hizo katika ukumbi wa  Karume House, Mjini Zanzibar.
Amesema mvua hizo zimesababisha mafuriko katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mjini Magharibi na kupelekea athari kubwa katika maeneo hayo ikiwemo vifo vya watu, uharibifu wa nyumba za makaazi na upotevu wa mali na mifugo.
Aidha Waziri Aboud amesema kuwa maiti ya mtoto imeshapatikana na kuzikwa jana Tarehe 3/5/2015 na maiti ya Nd. Juma Hamad bado haijapatikana na juhudi za kumtafuta zinaendelea.
Amefahamisha kuwa maeneo yaliyoathirika zaidi na mvua hizo ni pamoja na Magomeni, Jang’ombe, Nyerere, Sebleni, Sogea, Mwanakwerekwe, Welezo, Kisauni, Tomondo, Mombasa, Kinuni, Mtopepo, Chumbuni, Kwahani, Mpendae, Bububu na Kwaalinato, ambapo maeneo yote hayo yanapatikana ndani ya Mkoa wa Mijini Magharibi.
Ametanabahisha kuwa, kwa vile mvua bado zinaendelea kunyesha ni vyema wananchi wakachukua tahadhari ili kujiepusha na athari zaidi zinazoweza kujitokeza, ikiwemo wazazi kuangalia watoto wao na kuhakikisha hawachezi karibu na maeneo yanayotuama maji, kwa wale wanaoishi mabondeni ni vyema wakahama sehemu hizo.
Waziri Aboud pia amewataka wananchi waliochimba mashimo katika maeneo ya makaazi wawe waangalifu kwa kuyafunika haraka iwezekanavyo , kuchemsha maji wanayoyatumia, kuhifadhi chakula ili kuepukana na maradhi ya miripuko pamoja na kufuata kanuni za afya ikiwemo usafi binafsi na maeneo yanayowazunguka.
Vilevile amewataka wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu kwani Serikali itaendelea kushirikiana nao ili kuhakikisha kuwa hali ya maisha kwa wananchi hao inarudi kama kawaida pamoja na kuwapa pole wale wote waliopoteza jamaa na mali zao.


IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

Maji ya mvua yenye kasi yakitapakaa kila eneo la Zanzibar
Wananchi wakihangaika kwenye mafuriko kutokana na mvua 
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar nako kumefurika. Picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2015

    Poleni na mvua zilizoleta maafa, wataalam waangalie njia za maji ya mvua zimezibwa vipi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2015

    PICHA ZAIDI ULIZOWEKA MBONA SIZO??

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 05, 2015

    very poor town planning

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...