UMOJA wa Walemavu Wafanyabiashara  Mkoa wa Dar es Salaam (Uwawada),wamefunga barabara ya Uhuru na Kawawa kushinikiza serikali kutoa maelezo kuhusiana na  uvunjaji wa meza katika soko la Machinga Complex  unaodaiwa kufanywa na askari wa jiji usiku wa jana.

Wafanyabiashara hao wamekaa katikakati ya barabara kwenye makutano ya Barabara ya Uhuru na Kawawa  karibu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ikiwa na lengo kutaka maelezo ya serikali kuu juu kufanya operesheni usiku bila kufanya ushirikishaji kwa wahusika.

Akizungumza  na  waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kidumuke Kidumuke amesema meza za walemavu zilizopo machinga Compelex ziliwekwa kutokana na makubaliano na kuamuliwa kuweka meza hizo, lakini wamevunja utaratibu waliokubaliana, hivyo kuamua kufunga barabara bila utaratibu.

Kidumuke amesema kutokana uvunajaji huo walemavu baadhi wamepotelewa na mali zao na hakuna mtu ambaye atafidia, hivyo serikali inawajibika kulipa na makubaliano hayo yanatakiwa yawe katika maandishi.

"walemavu tumekuwa tukionewa kutokana na hali zetu lakini leo tunawapa usumbufu wananchi ni kwa ajili ya kutaka haki zetu na tunawataka radhi watusamehe". amesema Kidumuke.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Raymond Mushi amesema kuwa kuhusu fidia watafanya uchunguzi ili kuona kama kuna waliopotelewa na mali zao.

Mushi amesema walemavu watarudi katika maeneo hayo na waondoke eneo la barabara ili watu wengine waweze kufanikisha shughuli  zao.
 Umati wa watu ukionekana katika eneo la Makutano ya Barabara ya Kawawa na Uhuru, Karume jijini Dar es salaam kutokana na kuwepo kwa baadhi ya walemavu wa viungo waliokaa katikati ya Barabara hizo kuitaka kutokana na kuvunjwa kwa mabanda yao ya biashara na watu wasiojulikana katika eneo la  la Karume, hali iliyopelekea njia hizo kufungwa kwa muda na kuleta usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo.
Baadhi ya Walemavu wakijadiliana jambo huku wakisubiri hatma ya mgomo wao kutatuliwa.
Mmoja wa Walemavu akishiriki kwenye mgomo huo ambao mpaka sasa bado hatma yake haijafahamika rasmi.
Baadhi ya Walemavu wakijadiliana jambo huku wakisubiri hatma ya mgomo wao kutatuliwa.Globu ya Jamii itawaletea taarifa kamili kuhusiana na Mgomo huu wa Walemavu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...