Na Mwandishi Wetu 

MABONDIA Iddi Pialali wa Kiwangwa Bagamoyo na Adam Ngange wa Chanika Dar es salaam watapima uzito siku ya ijumaa katika stendi kuu ya mabasi Bagamoyo na kupigana siku ya jumamosi ya mei 16 katika ukumbi wa che kwa che uliopo Bagamoyo mjini, ambapo mabondia hao watamalizia ubishi wao wa nani zaidi kati ya Bagamoyo na Chanika.

Mpambano huo utakaosimamiwa na Chama cha Ngumi za Kulipwa P.S.T utakuwa wa raundi sita na kwa uzito wa kg 61, ambapo kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi siku hiyo yatakayowakutanisha bondia Rashidi Haruna atakumbana na Kaminja Ramadhani na Halid Hongo atakabiliana na Kishoki Mbishi, mpambano mwingine ni Abdallah Samata atakaye zidunda na Maono Ally.

Mapambano hayo yanaletwa kwenu na Sharif Promotion wakati mgeni rasmi siku hiyo ni bondia kutoka Morogoro, Cosmas Cheka ambaye atakuja kuwapa nasaha mbalimbali mabondia na mashabiki wa mchezo wa masumbwi kuweza kusonga mbele kwa mchezo huo mjini Bagamoyo

kingilia katika mpambano uho ni Tsh, 8000 kwa V.I.P na kwaida ni sh. 5000

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na upatikanaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar vs Manny Paquaio 2015 , Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakavyokuwa vikigawiwa na kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa ghalama nafuu kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa masumbwi nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...