Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh. Dkt. Seif Rashid ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kupitia Idara yake ya Tiba na Upasuaji Moyo kwa kufanikisha matibabu ya moyo kwa wagonjwa 24 katika kipindi cha siku nne. 

Hayo ameyasema alipotembelea Hospitali hiyo kuona namna ambavyo wataalam wetu kwa kushirikiana na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre iliyoko Riyadhi nchini Saudi Arabia ambao wamekuwepo Muhimbili toka tarehe 9 Mei na wanatarajiwa kuondoka tarehe16 Mei, mwaka huu.

Dkt. Rashid amesema ni mfanikio makubwa sana ambayo tumefikiwa hadi hivi sasa katika upasuaji moyo na tunatarajia kasi hii ya ushirikiano ikiendelea tutapunguza kwa kasi sana wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

“Kama ndani ya siku nne tu mmeweza kuziba matundu ya moyo kwa watoto 12 bila kufungua kifua na mkaweza kufungua vifua vya watoto wengine 12 ambao kutokana na hali zao walihitaji kufunguliwa vifua, mmenipa moyo sana kwamba mmejidhatiti kuhakikisha Watanzania wanapata huduma hii kwa haraka na kwa ufanisi wa hali ya juu, nawapongezeni sana” amesema Dkt. Rashid.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid ambapo kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hussein Kidanto wakiwa ndani ya Chumba chenye mtambo wa Cath Lab ambao unatumika kuzibua mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye moyo iliyoziba na pia mtambo huu pamoja na mambo mengine umetumika kwa mara ya kwanza kuziba matundu ya moyo bila kufungua kifua. Mtoto huyu ambaye jina lake limehifadhiwa anasubiri kuzibwa tundu kwenye moyo wake kwa kutumia mtambo wa Cath Lab. Ndani ya siku tatu ataruhusiwa kwenda nyumbani.
Hapa ni ndani ya chumba chenye vifaa vya kisasa kabisa kwa ajili ya wagonjwa wenye kuhitaji uangalizi maalumu (ICU) ambapo mtoto aliyefanyiwa upasuaji anaangaliwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 14, 2015

    Boresha utoaji huduma zaidi na zaidi hapo Muhimbili ili sis wananchi tunufaike hapa hapa nchini.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 14, 2015

    Hongera kwa hatua hii; Pia Kumbuka haki ya mgonjwa kupewa heshima anayosthairi "Privancy"- si vizuri kumwonyesha mngonjwa akiwa amelala au alikubali picha zake kuwekwa hadgarani (HEPA).

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...