BENKI ya NMB, imetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma vyenye thamani ya shilingi milioni 10 ikiwa na lengo la kusaidia uboreshaji wa huduma katika hospitali hiyo kubwa kwa mikoa ya kanda ya kati – Singida na Dodoma.
Baadhi ya vifaa vilivyotolewa ni magodoro 22 na mashuka 422 ambayo kwa maelezo ya mganga mkuu wa hospitali hiyo – Dr Ezekiel Mpuya vitasaidia sana kuweka mazingira rafiki kwa wagonjwa wanaolazwa hospitalini hapo hususani akina mama wajawazito na watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Kapteni Mtaaafu - Chiku Galawa (wa tatu kushoto) akipokea sehemu ya shuka 422 na godoro 22 yenye thamani ya shilingi Milioni 10 kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Kati - Gabriel ole-Loibanguti (kushoto). Vifaa hivyo vilitolewa na NMB kwaajili ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma katika hafla iliyofanyika kwenye kilele cha siku ya wauguzi duniani - Dodoma.
Meneja wa NMB Kanda ya Kati - Gabriel ole-Loibanguti (kushoto), akikabidhi sehemu ya magodoro 22 na shuka 422 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 10 kwa mkuu wa mkoa wa Dodoma Kapteni Mstaaafu - Chiku Galawa zilizotolewa na NMB kwaajili ya hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye silele cha siku ya wauguzi Duniani. Kulia ni Muuguzi Mkuu wa hospitali ya Dodoma - Anatolia Mkindo na kushoto ni Mganga Mkuu wa Hopsitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma - Ezekiel Mpuya
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...