SERIKALI imesema kutokana na Jiji la Mwanza kujengwa nyumba za kudumu bila mpangilio maalumu, imeanza mchakato wa kuainisha maeneo yote ya Wilaya ya Ilemela na Nyamagana yanayounda jiji hilo ili sehemu makazi, biashara, viwanda na huduma za jamii zifahamike.
Imesema kabla ya kuanisha maeneo hayo, leo itaanza kukutana na wadau wote na wananchi wa jiji hilo ili kupokea maoni na mapendekezo kabla ya kuanza utekelezwaji wa mpango huo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyolewa jana kwenye vyombo vya habari na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Faisal Issa,imesema mpango huo umelenga kuondoa migogoro ya ardhi na uvamizi wa maeneo yasiyoruhisiwa.
|
Home
Unlabelled
MPANGO MKAKATI WA KULIPANGA JIJI LA MWANZA KWA MIAKA 25 IJAYO WAWADIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hii hatua ni nzuri, kujenga miji kiholela kuna matatizo yake kwa wakazi.
ReplyDelete