Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

WAKALA wa nishati vijijini (REA) inaendelea kusambaza umeme katika vijiji vilivyobaki kwa awamu, kupitia mradi kabambe wa umeme vijijini ambao umelenga kuweka umeme maeneo ambayo yalikuwa mbali na huduma hiyo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA), Edmund Mkwawa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Mkwawa amesema kuwa mradi huo umeweza kutoa mafunzo na kuwajenga wajasiliamali mbalimbali wa nishati ya umeme vijijini kwa makundi 62 ambayo yalikuwa na wajasiliamali 1,494 ambao wamepewa mafunzo ya technolojia ya nishati jadidifu na utayarishaji wa mipango mbalimbali ya kibiashara.

Pia Mkwawa amesema kuwa katika mradi huo wamefunga mifumo ya umeme wa jua katika vijiji 82 vya Halmashauri ya Sumbawanga vijijini katika Shule za Sekondari, Zahanati,Vituo vya Afya pamoja na vituo vya Polisi na kuweka taa kwenye maeneo ya mikusanyiko ya shughuli za kijamii.

Wakala wa nishati vijijini (REA) pia wamehamasisha wajasiliamali katika sekta za Umma na sekta binafsi kushiriki katika Miradi katika utekelezaji wa miradi ya nishati nchini kwa kuanzisha shindano la Lighting Rural Tanzania Competition ambalo limekuwa likifanyika kila baada ya Miaka miwili.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA), Edmund Mkwawa (katikati), akisikiliza maswali kutoka kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, mara baada ya kutoa taarifa ya maendeleo ya miradi ya umeme vijijini,Kushoto ni Mkurugenzi wa Bodi ya REA, Dkt. Gideon Kaunda na Mkurugenzi Mkuu, Lutengano Mwakahesya.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...