Naibu Katibu Mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT)  Mhe. Ezekiah Oluoch akizungumza juu ya Uchaguzi Mkuu wa chama hicho kitaifa utakaofanyika Mei 28 katika mkutano Mkuu wa chama hicho utakaofanyika Mei 25 mpaka 28 katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Ngurudoto, jijini Arusha katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za mkoa za chama hicho. Kushoto ni Katibu wa chama mkoa Hassan Said

Na Woinde Shizza, 
Arusha
Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kinatarajia kufanya uchaguzi mkuu wa kitaifa May 28 mwaka huu ili kupata viongozi watakaokiongoza chama hicho kwa kipindi  cha miaka 5 pamoja na kutetea maslahi ya walimu.

Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Ezekiah Oluoch amesema kuwa nafasi zinazogombaniwa ni Mwenyekiti wa chama,Katibu,Naibu Katibu mkuu pamoja na Mhazini wa chama hicho.

Mhe. Oluoch  alisema hayo jana akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi za  chama hicho Mkoa wa Arusha kuwa hadi sasa wana jumla ya wanachama  452 wamejitokeza kugombea nafasi hizo  na nafasi nyingine ikiwamo Mwakilishi wa Walimu wenye ulemavu  ,na kitengo cha Walimu wanawake.

“Wagombea ni wengi na nafasi ni chache tumeona tuache hivyo maana yake tukizuia idadi tutakua tumeminya demokrasia” Alisema Ezekiah

Mhe. Oluoch  amesema kuwa jumla ya walimu 1000 wanatarajia  kushiriki uchaguzi huo wa kitaifa ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete.

Mwenyekiti wa Chama hicho  Mkoa wa Arusha (CWT) Jevin  Buruya amesema kuwa wamejiandaa vyema kwa ajili ya uchaguzi huo hivyo amewataka walimu wajitokeze kwa wingi katika uchaguzi huo.

Buruya  amesema kuwa Chama cha Walimu Tanzania kitafanya mkutano mkuu utakaoanza May 25 hadi 28 ambapo agenda kuu ni Uchaguzi Mkuu. Mkutano huo unatajwa kuwa Mkutano wa Mwisho wa Raisi Kikwete kuwahutubuia walimu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...