Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

MALENGO ya Milenia ya Nne na Tano yamefikiwa kutokana na mkakati wa kupunguza vifo vya Mama na mtoto nchini vinavyotokana na uzazi kwa robo tatu na kuweza kufikia wakina mama 193 kwa vizazi hai 100,000.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid wakati akitangaza kuwepo kwa Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yatafanyika kesho katika viwanja Mkendo mkoani Mara.

Amesema tafiti zilizofanywa katika nchi 72 zimeonyesha kwamba upatikanaji wa huduma mwafaka za ukunga umewezesha kupunguza kiwango cha vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi kwa wastani wa asilimia tatu kwa mwaka kuanzia mwaka 1990, jambo ambalo linaridhisha umuhimu wa wakunga katika kuhakikisha kwamba hakuna mama mjamzito anapoteza maisha kutokana na sababu zinazoweza kuzuilika.

Katika Maadhimisho hayo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi ambapo watu wa maeneo ya karibu wametakiwa kushiriki na kuweka kazi za wakunga katika utoaji wa huduma za uzazi.

Dk. Seif amesema kwa mujibu wa Shirikisho la Vyama Vya Wakunga Duniani,Mkunga akitayarishwa vizuri kwa kufuata viwango vilivyowekwa na kuzingatia mahitaji ya nchi,mkunga huyu anaweza kutoa asilimia 87 ya huduma zote muhimu anazohitaji mama mjamzito na mtoto mchanga.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Wakunga kwa Maendeleo ya Kizazi kijacho" ikiwa inalenga kauli hiyo kutambua umuhimu wa wakunga katika kuokoa maisha ya kina mama na watoto wachanga .

Amesema kuwa kutokana na kutambua umuhimu wa wakunga wameongeza idadi ya vyuo kutoka 3,000 hadi 10,000 ikiwa lengo lake kupunguza vifo vya mama mjamzito na mtoto mchanga.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza maadhimisho ya siku ya wakunga duniani iliyofanyika leo katika ukumbi wa Wizara ya Afya na Ustawi Jamii jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Utawi wa Jamii,Dk.Donnan Mbando akimkaribisha Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dk.Seif Rashid kutangaza Maadhimisho ya Siku ya Wakunga iliyofanyika leo katika ukumbi wa Wizara ya Afya na Ustawi Jamii jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakifatilia taarifa ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dk.Seif Rashid ya Siku ya Wakunga Duniani iliyofanyika leo katika ukumbi wa Wizara ya Afya na Ustawi Jamii jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Emmanuel Massaka).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...