UJENZI wa Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam ambayo Waziri wa Ujenzi, Dkt John Pombe Magufuli alikataa kuipokea mwaka 2011, baada ya kujengwa chini ya kiwango. Ujenzi wa kipande hicho cha kilomita 5.1 kutoka Mtongani hadi Mbagala Rangi Tatu, ulikamilika mwaka 2012. Mafundi wa Kampuni ya Kajima ndio waliokuwa wakijenga kipande hicho cha barabara . 
Dkt.  Magufuli alikataa kuipokea barabara hiyo kutoka katika Serikali ya Japan, iliyotoa msaada wa fedha na ujenzi kufanywa na Kampuni ya Kajima, baada ya kujiridhisha kuwa ilijengwa chini ya kiwango. 
Dkt. Magufuli alimweleza Balozi wa Japan nchini, Mhe. Masaki Okada kwamba asingeipokea barabara iliyo chini ya kiwango hata kama imetolewa kama msaada kwa Tanzania. 
 Baada ya msimamo huo wa Serikali, Japan ilifanya uchunguzi na kubaini kuwa kampuni hiyo ilijenga barabara hiyo chini ya kiwango. Kutokana na hali hiyo, Balozi Okada aliahidi kurudia ujenzi wa kilometa 5.1 kipande ambacho waligundua kuwa kampuni hiyo ilijenga chini ya kiwango. 
 Baada ya kauli hiyo ya Balozi, Dk Magufuli alimtaka mkandarasi huyo kuondoa tabaka la lami na kuweka tabaka jingine gumu lenye sentimita saba jambo ambalo limetekelezwa baada ya marudio.
Ujenzi wa Barabara ya Kilwa yenye urefu wa kilomita 13.5 kutoka bandarini hadi Mbagala Rangitatu ulizinduliwa kwa kuwekwa jiwe la msingi na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2007.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...