Familia ya marehemu mzee Japhet Mbaga, wa Dar es Salaam inasikitika kutangaza kifo cha mama yao, NENDIWE MBAGA, kilichotokea hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge, siku ya Jumatano mchana, tarehe 13 Mei 2015 kwa ugonjwa wa pneumonia. 
Mama Nendiwe ni mama mzazi wa MARY RUSIMBI, Hillary Mbaga, Michael Mbaga, Rose Mshana, Stella Mbaga na John Mbaga.
Mazishi yanatarajiwa kufanyika makaburi ya Kinondoni, siku ya Jumapili tarehe 17 Mei 2015 saa 10.00 jioni. 
Ratiba ya kutoa heshima za mwisho itafanyika siku hiyo hiyo, saa 7.00 mchana nyumbani kwa Mary Rusimbi (Mkurugenzi Mkuu, WOMEN FUND TANZANIA) eneo la Tabata, nyumba za TAZARA. 
Baadaye saa 9.00 Ibada ya kumuaga itafanyika Kanisa la KKKT Mwananyamala B.

"Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake na lihimidiwe."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...