Na Victor Mariki - Ofisi ya Makamu wa Rais
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais ( Mazingira), Dk.
Binilith Mahenge amesema kuwa Serikali inaendelea kukabiliana na changamoto za uharibifu wa mazingira kwa kuhamasisha utekelezaji wa mipango
ya kitaifa ya kuhifadhi mazingira pamoja na miongozo yake.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati
wa maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya
Mazingira Duniani ambayo hufanyika tarehe 5 Juni kila mwaka ambapo mwaka huu
maadhimisho hayo yatafanyika jiji la Milani nchini Italia kimataifa na kitaifa
yatafanyika mkoa wa Tanga.
Aidha Waziri Mahenge, alibainisha baadhi ya sababu za kuichagua
Tanga kuwa sehemu ya maadhimisho hayo ni
kutokana na changamoto za mazingira zinazoukabili mkoa huo ikiwemo uvuvi
haramu, uharibifu vyanzo vya maji, mmomonyoko wa fukwe pamoja na kuzama kwa visiwa vya Maziwe kutokana na mabadiliko ya tabianchi.
Aliongeza kuwa ujumbe wa
maadhimisho ya siku hiyo mwaka huu unasema " Ndoto Bilioni Saba.
Dunia Moja. Tumia Rasimali kwa Ungalifu." ambapo alifafanua kuwa ujumbe huo unahimiza
jamii katika umuhimu wa utumiaj endelevu wa rasimali kwa faida zao na kwa
kizazi kijacho kwa kuzingatia ongezo la watu duniani lilofikia bilioni saba kwa
sasa.
Sanjari na hayo Waziri Mahenge alitoa wito kwa kila mkoa
kutekeleza shughuli za kuhamasisha uhifadhi wa mazingira kwa kudhibiti uvunaji
miti, kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ya kuni na mkaa, kupanda miti inayofaa
kwenye vyanzo vya maji na kuvitaka viwanda vizingatie uzalishaji bora
utakaopunguza gesijoto na kuwa na mifumo
mizuri ya majitaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...