Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika, Karibiani na Pasifiki Balozi Dr Patrick Gomes (kushoto) akisalimiana Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala P baada ya kuzindua Utaratibu wa Uuzaji wa Filamu za Tanzania kwenye Mtandao. Uzinduzi huo humefanyika Makao Makuu ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki Jijini Brussels Ubeligiji.
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mheshimiwa Diodorus Kamala[kushoto] akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wageni waalikwa kutoka mataifa mbalimbali katika uzinduzi wa filamu za kitanzania ambazo sasa zitakuwa zikiuzwa online.sherehe hizo za uzinduzi ambazo zilifanyika jijini Brussel nchini Ubelgiji na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
Mwenyekiti wa Proin Group Tanzania ndugu Johson Lukaza akizungumza machache na kuwashukuru watu wote waliohudhuria uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania online hapo jana katika ukumbi wa ACP House jijini Brussel nchini Ubelgiji na kuudhuriwa na watu wa mataifa mbalimbali.Uzinduzi huo ulifanywa na balozi wa Tanzania Mheshimiwa Diodorus Kamala.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...