Na Mwandishi Wetu
Taasisi
ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyochini ya Wizara ya Fedha
(UTT-PID) ipo kwenye kushiriki maonyesho ya Nyumba na Makazi
yanayofahamika kama DAR PROPERTY 2015, yaliyoanza leo Mei 2 na
kutarajiwa kumalizika Mei 5, mwaka huu ndani ya ukumbi wa Diamond
Jubilee V.I.P Hall uliopo Upanga, Jijini Dar es Salaam.
Katika
maonyesho hayo, UTT-PID, inashiriki ikiwemo kutoa elimu mbalimbali
na maelezo juu ya utendaji wa kazi za taasisi pamoja na huduma kwa watu
mbalimbali wanaotembelea kwenye banda lao hilo ndani ya Diamond Jubilee
V.I.P Hall.
Aidha,
mapema leo Mei 2, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, alipata wasaha pia wa
kutembelea banda hilo la UTT-PID na kupata maelekezo kadhaa ya namna ya
utendaji wa kazi wa taasisi hiyo hapa nchini.
KAZI ZA UTT-PID
Kazi za UTT-PID ni pamoja na Utoaji huduma za ushahuri katika maeneo
ya upembuzi yakinifu wa miradi mbalimbali, Uratibu wa fedha na huduma
zinazohusiana katika maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au
taasisi za fedha, uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi ya
zabuni na usimamizi wa majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi
za usimamizi wa majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.
Dar Property 2015.
Ni
maonesho ya siku nne kuanzia Mei 2 hadi 5, ambayo wadau mbalimbali
kutoka Mashirika binafsi na Taasisi za Umma zinazojihusiha na uwekezaji
katika Majumba, Ardhi na Makazi wanashiriki. DAR PROPERTY, ambayo kwa
mwaka huu ni ya msimu wa pili yakifanyika na kushirikisha wadau hao
mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...