Na Profesa Mbele
Napenda kuendelea na jadi yangu ya kuvitaja vitabu nilivyoongeza katika maktaba yangu katika siku chache zilizopita. 

Kitabu kimoja ni The Poetic Edda: Stories of the Norse Gods and Heroes,kilichotafsiriwa na Jackson Crowford. The Poetic Edda ni kitabu maarufu sana ambacho nimekisikia kwa miaka mingi. Ni mkusanyo wa hadithi na mashairi ya mapokeo juu ya miungu na mashujaa wa Iceland.

Nimeamua kujipatia nakala wakati huu ambapo nimekuwa nafundisha utungo maarufu wa Finland uitwao Kalevala. Kwa pembeni nimekuwa nayapitia pia mashairi ya mapokeo ya Finland yaliyokusanya na Elias Lonnrot katika kitabu kiitwacho Kanteletar. Nina hamu ya kuona kama The Poetic Edda inahusiana na hizo tungo zingine, kwa kuzingatia kuwa zote ni za Ulaya ya kaskazini.

Kitabu kingine nilichonunua ni The Village by the Sea, cha Anita Desai wa India. Nilipangia kukifundisha muhula huu katika kozi yangu ya Post-colonial Literature, lakini tumeishiwa muda. Nimeshafundisha riwaya kadhaa za Anita Desai. Ni mwandishi bora sana. Ndio maana nikaamua kukiweka kitabu chake cha The Village by the Sea katika orodha ya muhula huu.

Kitabu kingine nilichonunua ni Monkfish Moon. Ni mkusanyo wa hadithi fupi za Romesh Gunesekera wa Sri Lanka, ambaye riwaya yake ya Reef nimeifundisha. Gunesekera ni mwandishi hodari sana. Nilikijumlisha kitabu chake chaMonkfish Moon katika orodha yangu ya Post colonial Literature. Lakini, muda umeshindikana.

Kitabu kingine nilichonunua, yapata wiki moja iliyopita, ni See Now Then cha Jamaica Kincaid wa Antigua, Carribean. Niliwahi kuhudhuria mhadhara wake katika Chuo Kikuu cha Minnesota.

Kitabu kingine nilichonunua, ambacho nimekipata leo, ni The Gunny Sack, cha Moyez Vassanji. Moyez Vassanji alizaliwa Kenya lakini alikulia Dar es Salaam. Ni mwandishi maarufu ambaye anaishi Canada. Kati ya vitabu vyake vinavyovuma sana ni Uhuru Street na The Book of Secrets., ambacho niliwahi kukifundisha katika semina ya waalimuChuo cha Colorado. Kinavutia sana kwa ustadi uliotumika katika kukiandika. Kitabu chake kingine, Amriika, nilikinunua miezi mingi iliyopita ila sijakisoma bado.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...