Na. Mwandishi Maalum
Wananchi wa Wilayani Same katika kata ya Hedaru, Makanya na Vunta wameishukuru serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya uratibu maafa, kwa kuwajengea uwezo wa kuzuia, kupunguza na kukabiliana na maafa yanayotokana na ukame ambao umekuwa ukizisumbua kata hizo Kutokana na mabadiliko ya Tabia Nchi.
Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Mradi wa kujengea jamii uwezo wa kukabili maafa ya ukame imefanikiwa kujenga uwezo huo kupitia vikundi vya maendeleo vya wilayani humo, ikiwa vikundi kumi (10) kutoka kata tatu za wilaya hiyo vimepatiwa Mbuzi 40, kuku 50, mbegu za mihogo, viazi, mtama, mboga mboga pamoja na kutoa miche ya miti kwa shule moja kila kata na vifaa vya kutunza bustani.
Akiongea wakati Idara hiyo ilipokuwa ikifuatilia utekelezaji wa mradi huo hivi karibuni, wilayani humo katika kata ya Makanya, kijijini Mgwasi, Mwenyekiti wa kikundi cha Kavangere, Stephano Hamisi, alieleza kuwa wananchi wa kata hiyo kupitia ufadhili wa mradi huo wameweza kulima na kufuga hali inayowajengea uwezo wa kupunguza na kukabiliana na maafa yanayotokana na ukame.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...