Vijana wakiwa katika Maandamano nchini Burundi
Watu wanne wamefariki dunia na wengine tisa
kujeruhiwa katika maandamano ya kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania Urais kwa Mhula wa tatu.
Mamia ya watu wamejitokeza kwenye maandamano hayo huku baadhi
wakichoma moto baadhi ya vitu katika nchi hiyo.
Siku ya jumanne Mahakama ya Katiba ilikubali kuwa Rais
Nkurunziza anaweza kugombea urais ambapo ilisema ni halali yeye kuwania tena
urais kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Katika hotuba yake siku ya jumatano Rais Nkurunziza alisema kama
atachaguliwa tena kuongoza nchi hiyo, mhula huu utakuwa wa mwisho kwake kuwa
madarakani.
Amani amani Burundi kutafuta kazi kwa wanasiasa kusisababishe mauaji.
ReplyDelete