Wateja wa Vodacom Tanzania sasa wameanza kunufaika na huduma mpya ya Ongea iliyozinduliwa rasmi leo ambayo inatoa unafuu mkubwa wa kupata huduma za mawasiliano kwa wateja na wananchi kwa ujumla. Ambapo mteja akinunua muda wa maongezi kwa Tsh 1,000/-mteja anapata dakika 100 za maongezi kupiga simu kwa mtandao wa Vodacom kwenda Vodacom,SMS 1000 na MB 100 za data.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hii mpya,Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa,amesema kuwa Vodacom itaendelea kuboresha huduma mbalimbali kwa wateja wake kwani kuna umuhimu wa kuwarahisishia mawasiliano wateja ili wapate kufanya kazi zao kiurahisi zaidi. Alisema jinsi ya kujiunga na huduma hii mpya ni rahisi sana,Wateja wanatakiwa kupiga namba *149*01# .Pia  wataendelea kunufaika na huduma nyingine kama vile vifurushi vya cheka .

“Kwa mara nyingine Vodacom imewaletea  huduma ya ongea wateja wake ili kuwawezesha  kupata huduma za mawasiliano kwa urahisi zaidi  kwa kutuma ujumbe wa maneno kwa gharama nafuu ikiwemo pia kuwawezesha kuperuzi interneti kwa gharama ya chini.Huduma hii inawahusu watumiaji wa mtandao wa Vodacom tu”Alisema Twissa.

Dunia ya leo inahitaji kila mtu awasiliane na mwenzake na wapendwa wao kwa hivyo ni muhimu kuwawezesha kuwasiliana kwa bei nafuu na kwa urahisi zaidi. “Ongea itawawezesha Wateja wa Vodacom kuweza kuwasiliana zaidi na kuunganishwa popote pale walipo na kuinua uchumi wa nchi kupitia mawasiliano murua”. Alisema Twissa.

Vodacom Tanzania imekuwa ikibuni huduma bora zenye gharama nafuu za kuwarahisishia mawasiliano wateja wake ambapo mwaka jana ilizindua huduma ya Bonga iliyowezesha wateja kupiga simu kwenda mitandao yote Tanzania kwa Tsh 1.5 kwa sekunde.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...