Wizara ya afya na ustawi wa jamii  imesaini mkataba wa kuboresha huduma za ufundi wa vifaa tiba ili kusimamia matumizi bora na kutunza rasilimali,hivyo kumehitajika kuweka juhudi za maksudi kuandaa wataalam wa ufundi wa vifaa tiba kwa kuwajengea uwezo katika kufahamu namna ya matengenezo ya mashine zilizopo na zinazo endelea kununuliwa.

 Pia kuwapa   vitendea kazi(tools kits, measuring and calibration equipment) vyenye kuwezesha mafundi kuhakiki ubora wa ufanyaji kazi kwa baadhi ya vifaa tiba mara baada ya kufanyiwa matengenezo.

"Kwa ushirikiano huu kati yetu na Korea ya Kusini ikiwa ni nchi iliyopiga hatua kubwa kiuchumi na teknolojia au miundombinu kwa ujumla wake ninaimani tutajifunza mambo mengi na kutoa mchango mkubwa katika kuboresha huduma za afya hapa nchini".

Alisema kikubwa wamelenga kupata ujuzi zaidi kutoka kwao, ingawa watagharimia masuala mengi katika mchakato mzima. 

"Tunahitaji sisi wenyewe serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Afya, Manispaa na Halmashauri zote nchini kuhakikisha vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za Afya vinapatikana na vinatumika kutoa huduma kwa wagonjwa muda wote vinapohitajika,"alisema na kuongeza kuwa  hilo litawezekana kama  itatengwa bajeti za matengenezo kinga (Planned Preventive maintenance) na kutumia wataalam wa ufundi wa vifaa tiba wanaotambulika ".

 Naibu meneja wa Korea Foundation for International Health ( KOFIH) Gong, In Gyung wa korea ya kusini akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kusaini mkataba wa makubaliano ya ushiriki katika kuboresha huduma za ufundi wa vifaa tiba hapa nchini.Kulia ni katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donnan Mmbando.
 Dkt. Mmbando akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mkataba huo  toka serikali ya korea ya kusini katika kutoa mafunzo kwa mafundi wa vifaa na vifaa tiba walioajiriwa katika vituo vya kutolea huduma za Afya hapa nchini ili waweze kuongeza ujuzi katika matengenezo na kuboresha huduma ya ufundi.Kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Otilia Gowele
 katibu mkuu Wizara ya Afya na ustawi wa Jamii na Naibu Meneja toka KOFIH wakisaini mkataba huo. Mkataba huo  utasaidia pia  kuboresha huduma za ufundi wa vifaa tiba katika karakana za ufundi wa vifaa tiba zilizopo katika hospitali za rufaa za kanda, rufaa za mikoa na hospitali za wilaya
 Dkt. Mmbado akikabidhiwa mkataba huo toka kwa Naibu Meneja Gong, In Jae.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...