
Na Mwandishi Maalum
Bodi
ya Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyo chini ya Wizara
ya Fedha (UTT-PID), pamoja na Menejimenti yake iliyozuru nchini China
katika ziara maalum ya siku tano kwa ajili ya Mafunzo na kubadilishana
uzoefu imefana na tayari bodi hiyo imerejea nchini.
Katika
ziara hiyo, Bodi ya UTT-PID, ikiongozwa na mwenyekiti wake Mrs. Elipina
Mlaki pamoja na Menejimenti nzima walieleza kuwa imeweza kuwa ya
mafanikio makubwa huku wakiahidi kuyafanyia kazi yae yote waliojifunza
nchini China.
Katika
ziara hiyo, bodi na menejimenti ya UTT-PID walipata wasaha wa
kutembelea maeneo mbalimbali ya miji ya nchi hiyo ikiwemo makampuni
makubwa na kujifunza na kujenga na kudumisha ushirikiano wa utendaji wa
kazi.

Mwenyekiti
wa Bodi ya UTT-PID, Mrs. Elpina Mlaki (wa pili kulia) akilezea jambo
katika moja ya mkutano wao waliofanya katika ziara hiyo nchini China.
Anayemfuatia ni Mkurugenzi Mkuu wa UTT-PID, Dr. Gration Kamugisha
pamoja na wajumbe wa bodi na Menejimenti ya UTT-PID, Wengine kushoto ni
watendaji kutoka kampuni ya Chengdu Engineering Corperation ya nchini
humo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...