KATIKA
kuhakikisha kuwa msikilizaji wa Efm kupitia kipindi chake cha Joto la Asubuhi
anapata taarifa za kutosha na zilizosheheni masuala mbalimbali ya Kijamii, kuanzia
Juni 29, Jumatatu, kitakuwa na habari kutoka mikoa mbalimbali nchini katika
kipengele cha kona zote.
Msimamizi Mkuu wa Kipindi hicho Dennis Ssebo
ameitonya Blog ya Jamii kuwa tofauti na utaratibu wa kuripoti matukio
uliozoeleka Joto la asubuhi litakuwa likizimulika na kuzichambua habari hizo
zilizoandikwa na wabobezi wa mambo katika tasnia ya habari kuanzia saa kumi na
mbili hadi saa kumi na mbili na nusu asubuhi.
Joto la asubuhi ni kipindi cha asubuhi ambacho
kinaruka hewani kupitia 93.7 EFM kila siku Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa
kumi na mbili hadi saa tatu kamili asubuhi chini ya watangazaji wake mahili
Dennis Ssebo na Adella Tillya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...