MKUU wa wilaya ya Tarime Mkoani Mara, Glorious Luoga, (Katikati), akinyanyua juu mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 800, baada ya kukabidhiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampouni ya Acacia, Brad Gordon, (kushoto), katika hafla fupi iliyofanyika kwenye lango la kushukia kutyoka kilele cha Mlima Kilimanjaro, Mweka, Juni 28, 2015.
Fedha hizo ambazo ni kwa ajili ya kusaidia sekta ya eli kwa watoto kutoka familia duni, zimetokana na wafanyakazi wa Acacia na familia zao pamoja na marafiki, kupanda Mlima Kilimanjaro kwa nia ya kuchangisha fedha chini ya mpango wa kampuni hiyo wa "CanEducate".
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...