Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Angela Kairuki ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa ‘Viongozi Wanawake Vijana Wanaochipukia’ uliondaliwa na Taasisi ya UONGOZI kwa kushirikiana na Mfuko wa Wanawake Tanzania mapema leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulilenga kuzungumzia suala la wanawake na uongozi, na namna ya kutatua changamoto wanazozipata katika kufanikisha ndoto zao za kiuongozi katika sekta mbali mbali nchini.

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Institute Prof. Joseph Semboja akitoa neno la utangulizi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa ‘Viongozi Wanawake Vijana Wanaochipukia’ uliondaliwa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na Mfuko wa Wanawake Tanzania mapema leo jijini Dar es Salaam.
 Mbunge wa Viti Maalum ambaye pia ni Rais wa VICOBA Mh. Devota Likokola akichangia katika mjadala uliohusu wanawake na changamoto zao wanazozipitia katika kufanikiwa kutimiza ndoto zao, na namna ambavyo wanaweza kupita changamoto hizo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake Tanzania Bi. Mary Rusimbi (kushoto) akichangia akiendesha mjadala wakati wa mkutano wa ‘Viongozi Wanawake Vijana Wanaochipukia’ uliondaliwa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na Mfuko wa Wanawake Tanzania mapema leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa ‘Viongozi Wanawake Vijana Wanaochipukia’ katika picha ya pamoja. Walioketi kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Anna Maembe, Mhadhiri wa wa MUHAS Dk. Ave-Maria Semakafu, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mh. Eusebia Munuo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake Tanzania Bi. Mary Rusimbi na Mbunge wa Viti Maalum ambaye pia ni Rais wa VICOBA Mh. Devota Likokola.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...