Balozi, Patrick Chokala akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutangaza nia ya kugombea nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,
Globu ya Jamii
Globu ya Jamii
Mwandishi wa Habari wa Rais wa awamu ya Pili, BaloziPatrick Chokala ametangaza nia ya kugombea
urais ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ili aweze kupeperusha bendera hiyo
katika uchaguzi mkuu ujao mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Ukumbi
wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Balozi Chokala amesema umefika
wakati wa kurejesha haki kwa wananchi ili wawe na imani na uongozi na pia kuwa
na ari ya kuleta maendeleo.
Amesema katika kutekeleza miradi inapaswa kutumia
watalaam wa elimu ya jamii kikamilifu kabla ya kutekeleza kama mradi wa gesi
ambao ilileta vurugu katika mikoa ya Kusini wakati serikali ilikuwa ina nafasi
ya kuelewesha wananchi.
“Nimekuwa na uzoefu wa kutosha kuwafahamu watanzania
kwa miaka 13 nimekuwa Ikulu na pia nchi za nje nilizofanya kazi mfano Nigeria
na Urusi”amesema Balozi Chokala.
Chokala atakuwa ni mtu wa 38 kama atachukua fomu
katika kinyanganyiro cha urais katika Chama cha Mapinduzi (CCM).
Wakati wengine wanatangaza nia zao baadhi ya
wagombea katika nafasi hiyo ya CCM wanamaliza kutafuta wadhamini katika mikoa
mbalimbali.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...