Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akimsikiliza kwa makini, Diwani wa Nyakafulwa, Mathias Nyororo, aliyekuwa akifafanua kutoanza kwa mradi wa maji kijiji cha Masumwe, licha ya Rais Jakaya Kikwete kutoa fedha za mradi huo kiasi cha milioni 200,miezi sita iliyopita.Ufafanuzi huo ulitokana na baada ya wananchi kulalamika kutopata maji katika kijiji hicho katika mkutano wa hadhara ambao Kinana aliufanya katika kata ya Masumbwe, utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Masumbwe wilayani Mbongwe,mkoani Geita.
Baadhi ya Wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara uliokuwa ukifanyika katika uwanja wa Masumbwe,wilayani Mbogwe mkoani Geita.
Nape
Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwahutubia maelfu ya wananchi
katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Masumbwe wilayani
Mbogwe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kumwaga zege katika zahanati ya kijiji cha Kasheko kata ya Lulembera wilayani Mbogwe mkoani Geita.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa wodi ya akina mama inayojengwa kwa nguvu za wananchi katika kata ya Lugunga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Mganga Mkuu wa kituo cha afya cha Masumbwe wilayani Mbogwe,Dkt John Mgosha,alipokagua kituo hicho na kuwasha umeme wa REA kituoni hapo,kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.Kinana na ujumbe wake yupo katika ziara ya kikazi wilayani humo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2010-2015 inayotekelezwa na serikali.
PICHA NA MICHUZI JR-MBOGWE, GEITA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...