Makamu Mkurugenzi Mkuu wa Benki M, Bi. Jacqueline Woiso (pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati Bank M ikitangaza kushirikiana na Taasisi ya kibiashara ya Marekani ya hapa Tanzania (AMCHAM-TZ) katika kuwasaidia wanaosaka ajira katika kuzikabili changamoto za ajira kisasa zaidi. Wengine pichani toka kushoto ni Makamu wa Rais wa sasa wa AMCHAM-TZ,Bhakti Shah, Mkurugenzi Mkuu wa AMCHAM-TZ, Richard Miles, Bw. David Mbumila kutoka Restless Development na Peter Shiras kutoka Int'l Youth Foundation.
Mkurugenzi Mkuu wa AMCHAM-TZ, Richard Miles (pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza kushirikiana na Bank M katika kuwasaidia wanaosaka ajira katika kuzikabili changamoto za ajira kisasa zaidi.
Bank M leo imetangaza kuwa itashirikiana na Taasisi ya kibiashara ya Marekani ya hapa Tanzania (AMCHAM-TZ) katika kuwasaidia wanaosaka ajira katika kuzikabili changamoto za ajira kisasa zaidi.
AMCHAM-TZ imeandaa semina ya siku moja nzima ijulikanayo kama “DARAJA LA MAFANIKIO” (Bridge to Success) itakayofanyika tarehe 22 Juni mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam. Semina hii italenga kuwasaidia Watanzania kuongeza ujuzi wa namna ya kutafuta kazi na pia watapata mwongozo kutoka kwa maafisa rasilimali watu kutoka katika makampuni na taasisi kubwa zinazoheshimika katika nyanja mbalimbali. Semina hii inatarajiwa kuhudhuriwa na watu wapatao 4,000 wakiwamo wasomi mbalimbali waliomaliza masomo yao hivi punde pamoja na wataalamu mbalilmbali.
Akiongea na waandishi wa habari, mkurugenzi mkuu wa AMCHAM-TZ bwana Richard Miles alisema “Tanzania ina nafasi nyingi za ajira ambazo hazijatumika, hususani kwa vijana na wale wanaotafuta ajira kwa mara ya kwanza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...