Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
ALIYEKUWA Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa,Dk. Augustine Mahiga ametangaza nia ya kugombea urais ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), jijini Dar es salaam leo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Mahiga amesema maadili yamemomonyoka na kufanya kuwepo kwa rushwa na ufisadi.
Mahiga amesema ubadhirifu na ufisadi katika taifa kunahitajika kuwepo kwa mwelekeo katika kuweza kupambana na vitu hivyo ili maendeleo yapatikane kwa wananchi.
“Nikipata nafasi hii nitatumikia watu katika kuujenga uchumi imara kwa kila mwananchi kutokana na kuwepo kwa dira na kuondoa matabaka yanayotokana na ubadhirifu wa mali za umma”amesema Mahiga.
Amesema CCM itoe fursa, isifikie utawala wa watu wenye pesa hiyo sio dhamira ya CCM, na watu wanaotoa msaada uwe na kikomo chake.
Mahiga amesema katika kuweza kufikia uchumi wa kati kunatakiwa kupambana na rushwa na ufisadi, bila kufanya hivyo uchumi huo hautafikiwa.
Aliyekuwa Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Augustine Mahiga akizungumza wakati akitangaza nia ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.
Hii foleni ya uraisi ni ndefu na inazidi kuongezeka.
ReplyDeleteWacha waongezeke kama na wewe umelipia kadi na umejiangalia ukaona unatosha kuongoza watanzania zaidi ya milioni 45 tangaza nia tukisikie halafu kachukue fomu kabla muda haujaisha.
ReplyDelete