Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr, Titus Kamani, (kulia) akisalimiana na Meneja Uendeshaji na Huduma kwa wateja wa benki ya Exim Tanzania tawi la Babati mkoani Manyara Bw. John Ndyebonera ,alipotembelea kwenye banda la maonyesho la benki hiyo ambayo ilishiriki kwenye maadhimisho ya 18 ya wiki ya maziwa yaliyofanyika kitaifa wilayani Babati hivi karibuni. Wengine ni wafanyakazi pia wa benki hiyo.
 Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr, Titus Kamani, (kulia) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea kwenye banda la maonyesho ya benki ya Exim Tanzania tawi la Babati mkoani Manyara ambayo ilishiriki kwenye maadhimisho ya 18 ya wiki ya maziwa yaliyofanyika kitaifa wilayani Babati. Anayeshuhudia kwa karibu zaidi ni Meneja Uendeshaji na Huduma kwa wateja wa benki hiyo tawi la Babati  Bw. John Ndyebonera. Wengine pia ni wafanyakazi wa benki hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania tawi la Babati mkoani Manyara wakiongozwa na Meneja Uendeshaji na Huduma kwa wateja wa benki hiyo tawi la Babati  Bw. John Ndyebonera (Wa pili kulia), kwa pamoja wakishuhudia mmoja wa washiriki wa maonyesho ya 18 ya wiki ya maziwayaliyofanyika kitaifa wilayani Babati (wa kwanza kulia) akisaini kitabu cha wageni waliotembelea banda la maonyesho ya benki hiyo ambayo pia ilishiriki maonyesho hayo kwa mafanikio makubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...