Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje kutoka Wizara ya Nishati na Madini (Kushoto) akijadiliana jambo na Mtaalam mwelekezi kutoka Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya Nchini India, Sujit Kumar Singh (Kulia) kwenye mafunzo yaliyoshirikisha wakaguzi wa migodini nchini yaliyofanyika mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo yaliyoshirikisha wakaguzi wa migodini nchini yaliyofanyika mjini Bagamoyo mkoani Pwani wakishiriki katika zoezi la kuandaa mpango wa mazingira kwa vitendo katika mafunzo hayo.
Na Greyson Mwase, Bagamoyo
Taasisi ya Sayansi na Mazingira kutoka nchini India (Centre for Science and
Environment) kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini, imekamilisha
mafunzo ya siku nne yaliyoshirikisha wakaguzi wa migodi nchini ambapo wakaguzi
walijifunza jinsi ya kuandaa miongozo mbalimbali kwa ajili ya kutumika kwenye
ukaguzi wa mazingira kwenye migodi.
Akizungumza katika mahojiano maalum wakati wa mafunzo hayo, Kamishna
Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje alisema lengo la mafunzo hayo
lilikuwa ni kuwapa uelewa wakaguzi wa mazingira na migodi nchini wa kuandaa,
kuchambua na kupitia taarifa za athari kwenye mazingira kutokana na shughuli za
uchimbaji wa madini.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...