Zanzibar, Benki
ya Exim Tanzania imeahidi kuunganisha nguvu zaidi na mamlaka za
kimichezo visiwani Zanzibar katika kuhakikisha sekta ya michezo visiwani
humo inakua zaidi.
Hatua
hiyo ya benki ya Exim ilitangazwa na Meneja wa tawi la benki hiyo
visiwani humo Bw.Mwinyimkuu Said Ngalima wakati wa kilele cha mashindano
ya soka yaliyolenga kuibua vipaji vya mchezo huo yaliyohitimishwa
kwenye Uwanja wa Abeid Amani Karume, wilayani Mwanakwerekwe kwa udhamini
wa benki hiyo.
“
Kutokana na jitihada zinazoonyeshwa na mamlaka za michezo sambamba na
Serikali tumeona na sisi pia tuna haja ya kuunga mkono jitihada hizi
hasa katika kuibua vipaji ikiwa ni sehemu ya mpango wetu wa kushirikiana
na jamii.’’ alisema Bw. Ngalima.
Benki
hiyo ilikabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi tofauti ikiwemo seti
mbili za jezi kwa timu zilizoingia fainali, zawadi kwa mchezaji bora,
goli kipa bora na muamuzi bora. Pia benki hiyo ilitoa zawadi kwa
mchezaji aliyeonyesha kipaji zaidi.
Fainali
hiyo ilivutia mashabiki wengi wakiwemo viongozi wa serikali wilayani
humo na maeneo jirani wakiongozwa na Waziri wa Kazi na Huduma za jamii,
Mh.Ali Suleiman ambapo hadi mwisho wa mchezo timu ya Feza iliibuka na
ushindi wa goli 1-0 dhidi ya wapinzani wao timu ya Kid Boys.
Akizungumza
mara tu baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi Mh. Suleiman mbali na
kuipongeza benki ya Exim kwa udhamini wa mchezo huo pia alitoa wito kwa
mashirika na taasisi mbalimbali kujitokeza kwa wingi ili kusaidia sekta
ya michezo visiwani humo.

Meneja wa benki ya Exim Tanzania tawi la Zanzibar Bw. Mwinyimkuu Ngalima akimkabidhi seti ya jezi mwakilishi kutoka timu ya soka yaa Kid Boys ya visiwani humo ikiwa ni sehemu ya udhamini wa mashindano yaliyolenga kuibua vipaji vya mchezo huo yaliyohitimishwa kwenye Uwanja wa Abeid Amani Karume, wilayani Mwanakwerekwe hivi karibuni.
Waziri
wa Kazi na Huduma za jamii, Zanzibar Mh.Ali Suleiman (mwenye suti ya
kaki) akikabidhi kikombe cha ushindi kwa Nahodha wa timu ya soka ya Feza
ambayo ilifanikiwa kuibuka mshindi kwenye mashindano yaliyolenga kuibua
vipaji vya mchezo huo yaliyohitimishwa kwenye Uwanja wa Abeid Amani
Karume, wilayani Mwanakwerekwe hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni baadhi ya
maofisa kutoka benki ya Exim Tanzania (wadhaamini) pamoja na waandaaji
wa mashindano hayo.
Baadhi
ya Maofisa kutoka benki ya Exim Tanzania, wakisalimiana na wachezaji wa
timu ya soka ya Kid boys ya visiwani Zanzibar kabla ya kuanza kwa
mchezo uliozikutanisha timu hiyo dhidi ya timu ya Feza ya visiwani humo
pia kwenye mashindano yaliyolenga kuibua vipaji vya mchezo huo
yaliyohitimishwa kwenye Uwanja wa Abeid Amani Karume, wilayani
Mwanakwerekwe hivi karibuni. Timu ya Feza ilibuka na ushindi wa 1-0
dhidi ya Kid boys.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...