Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake cha leo pamoja na mambo mengine kilipitia mwenendo wa timu ya Taifa (Taifa Stars) ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya Tanzania na Uganda, kama sehemu ya tathmini ya mwenendo wa timu.
Kamati ya Utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo;
1. Ajira ya Kocha Mkuu Maart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia Juni 21, 2015.
2. Benchi lote la ufundi la Taifa Stars limevunjwa kuanzia Juni 21, 2015.
3. Uongozi wa TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA
MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Juni 20, 2015
Juni 20, 2015
sio mchezo tunaona akisindikizwa na wanamuziji mashuhuri kina Ras Makunja wakiwa na magitaa yao
ReplyDeleteBwana Nooij alisakiziwa na aliyataka mwenyewe. Alitupiwa wachezaji wa maboresho akawapokea. Waliisambaratisha timu ya taifa ya vijana na kutimulia mbali makocha akawachekea tu.
ReplyDeleteLeo wanajifanya wamefanya uamuzi mgumu.
Ndugu Malinzi na timu yako ya uongozi, inaonekana kazi imewashinda. Toka muingie madarakani TZ haijawa na chochote cha kujivunia kwenye medani ya mpira wa miguu. Please do something, we want results sio siasa-Mbongo mwenye machungu na gadhabu nyingi tu!
ReplyDelete