Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake cha leo pamoja na mambo mengine kilipitia mwenendo wa timu ya Taifa (Taifa Stars) ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya Tanzania na Uganda, kama sehemu ya tathmini ya mwenendo wa timu.

Kamati ya Utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo;
1. Ajira ya Kocha Mkuu Maart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia Juni 21, 2015.
2. Benchi lote la ufundi la Taifa Stars limevunjwa kuanzia Juni 21, 2015.
3. Uongozi wa TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA 
MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Juni 20, 2015

Kocha Mkuu wa Taifa Stars Maart Nooij akisindikizwa na ulinzi mkali usiku huu baada ya kumalizika kwa mchezo wa Tanzania na Uganda wa kuwania kufuzu fainali za CHAN katika Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar ambapo Taifa Stars ilichapwa 3-0.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2015

    sio mchezo tunaona akisindikizwa na wanamuziji mashuhuri kina Ras Makunja wakiwa na magitaa yao

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 21, 2015

    Bwana Nooij alisakiziwa na aliyataka mwenyewe. Alitupiwa wachezaji wa maboresho akawapokea. Waliisambaratisha timu ya taifa ya vijana na kutimulia mbali makocha akawachekea tu.
    Leo wanajifanya wamefanya uamuzi mgumu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 21, 2015

    Ndugu Malinzi na timu yako ya uongozi, inaonekana kazi imewashinda. Toka muingie madarakani TZ haijawa na chochote cha kujivunia kwenye medani ya mpira wa miguu. Please do something, we want results sio siasa-Mbongo mwenye machungu na gadhabu nyingi tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...