CV YA JUDGE
RAMADHANI
Nimezaliwa Desemba 28, mwaka 1945 Zanzibar
mjini nikiwa ni mtoto wa pili kati ya watoto wanane, wa kike wanne na wanaume
wanne. Ni Mkristo wa dhehebu la Anglikana.
Nimesoma shule mbalimbali za msingi Mpwapwa
mkoani Dodoma 1952 -1953 nikaenda Town School-Tabora nikasoma darasa la tatu
hadi la nne mwaka 1954-1956 na darasa la sita na saba nilisoma Kazel Hill sasa
inatwa Shule ya Msingi Itetemia mwaka 1957-1958. Na darasa la nane tu mwaka
1959 nikarudi kusoma Mpwawa.
Mwaka 1960-1965 nilijiunga na Tabora School
kwa ajili ya masomo ya kidato cha kwanza hadi cha sita. Kwakuwa nilifaulu nilichaguliwa
kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1966, na nilisoma shahada yangu
ya Sheria na ilipofika Machi 1970 nilihitimu masomo.
Na mwishoni mwa Machi mwaka huo huo wa 1970
nikajiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), niliingia jeshini kama
mwanasheria raia mpaka kipindi cha mafunzo ya kijeshi nikaenda kwenye mafunzo
na kisha nikarudi kuitumikia JWTZ.
Ilipofika mwaka 1971 nikapewa kamisheni kambi
ya Mgulani nikawa Luteni (nyota mbili). Nikaendelea na jeshi hadi mwaka 1977,
nikahamishiwa Brigedi ya Faru-Tabora nikiwa na cheo cha Meja.
Sasa mwaka 1978, wewe mwandishi ulikuwa
hujazaliwa, ndiyo mzee Aboud Jumbe Mwinyi, wakati huo akiwa ni rais akaniita
Zanzibar na kuniteua kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar na
kipindi hicho Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa ni Jaji wa Mahakama ya
Rufaa, Damian Lubuva.
Aidha Oktoba 1978 niliteuliwa kuwa Jaji Mkuu
wa Zanzibar. Na ilipofika Machi 1979 nilirudishwa JWTZ na baada ya muda mfupi
nikapelekwa kwenye vita ya Uganda , nikiwa na cheo cha Luteni Kanali na kwenye
vita hiyo nilikuwa naendesha mahakama za kijeshi.
Vita ilipokwisha nikarudi Zanzibar. Januari 8
mwaka 1980 nikaapishwa kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar, wakati huo nikiwa na cheo
cha Luteni Kanali. Nikaendelea na Ujaji Mkuu Zanzibar hadi Septemba 1989
alipoapishwa Jaji Mkuu Zanzibar Hamid Mahamod Hamid.
Hata hivyo Juni 23 mwaka 1989 niliteuliwa kuwa
Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania hadi mapema wiki hii nilivyoteuliwa kuwa
Jaji Mkuu wa Tanzania.
Nilipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani
hapa Bara ndiyo sababu ya kuacha ujaji Mkuu Zanzibar.
Januari 1993 niliteuliwa kuwa Makamu
Mwenyekiti katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na niliendelea na nafasi hiyo
hadi Januari 2003 na Oktoba 2002 niliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ambapo kipindi changu cha miaka mitano katika
tume ZEC kinamalizika Oktoba mwaka huu.
Novemba 2001, niliteuliwa kuwa Jaji wa
Mahakama ya Afrika Mashariki nafasi ambayo natakiwa nimalize kipindi changu cha
miaka sita Novemba mwaka huu.
Nina mke mmoja ambaye Mungu ametujalia
tumebahatika kupata watoto wanne, wawili ni wasichana na wawili ni wavulana.
Mtoto wangu wa kwanza anaitwa Francis (30)
huyu ni mwanasheria na anafanyakazi ya uwakili Manchester, Uingereza, Brigeth,
huyu ana shahada ya Uandishi wa Habari na anafanyakazi ICAP hapa nchini, Marina
ni mfamasia, yuko Liverpool, Uingereza na Mathew naye ni mfamasia, anafanya
kazi Liverpool.”
presidential material - very clean.
ReplyDeletesikujua kama alikuwa military officer...
NiTAMPIGIA kura .mdau USA nitarudi nchini ku kupigia kura .JAJI Anapiga kinanda kanisa la St Andrews .Sio mchezo baba mtu wa Mungu .Baba ake alikuwa askofu Mkuu kanisa la Anglicana.Baba poa Huyu
ReplyDelete