Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Mhe. Fatma Abdulhabib Fereji
amesema dawa za kulevya ni janga la Kidunia linalopigwa vita na
Mataifa yote Duniani.
Hayo
ameyaeleza huko Kiwanja cha Kombawapya Zanzibar katika Maaadhimisho ya
kupiga vita Utumiaji na Usafirishaji pamoja na Udhalililshaji wa Dawa
za kulevya Duniani.
Amesema
Zanzibar inakadiriwa kuwa na watumiaji wa dawa za kulevya zaidi ya 9000
idadi ambayo ni kubwa ukilinganisha na visiwa hivyo pamoja na idadi ya
wakaazi wake jambo ambalo linahatarisha maisha ya vijana kujiingiza
zaidi katika utumiaji huo
Aidha
amesema Seikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Tume ya Kitaifa ya
Kuratibu na Kudhibiti Dawa za kulevya chini ya Ofisi ya Makamo wa Kwanza
wa Rais huadhimisha siku hiyo kila Mwaka kwa lengo la kuitanabahisha
Jamii kuwa Dawa hizo ni janga la Kitaifa lisilovumilika hivyo
linahitaji nguvu na maarifa ili kupambana na janga hilo.
Hata
hivyo Waziri huyo amesema kuwa Zanzibar ni sehemu ya Dunia inayounga
mkono juhudi za Mataifa na Jumuiya mbalimbali za Kimataifa katika kupiga
vita Dawa hizo ambazo kwa asilimia kubwa zinaathiri nguvu kazi ya Taifa
lolote Duniani hasa vijana wenye umri mdogo wakiwemo Wanafunzi.
Rais wa watoto Tanzania Ameir Haji Khamis akitoa ujumbe wa watoto na
dawa za kulevya kwenye sherehe za siku ya kupambana na usafirishaji na matumizi
ya dawa za kulevya Duniani katika kiwana cha Kombawapya.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Ferej akitoa nasaha
katika maadhimisho ya siku ya kupambana
na usafirishaji na matumizi ya dawa za kulevya Duniani katika kiwanja
Kombawapya Mjini Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...