Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la kukaribisha mwezi mtukufu wa
Ramadhan wakibadilishana mawazo nje ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa
Mwalimu Julius Nyerere kabla ya Kuingia Ndani ya Ukumbi huo ili kujadili Kauli Mbiu ya Ndoa Chanzo
Cha Utu wetu Jana 14.06.2015.
Baadhi ya wataalamu wa Kiislam wakimsilizi kwa Makini Dr Ahmad Totonji
Kutoka Suadi Arabia alipokuwa akiwakilisha Mada ya Taasisi ya Ndoa, Jana, leo
na Kesho Katika Kongamano la Kukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Dr.
Totonji amewasihi waislam wataalamu kuwa
chachu ya mfano wa Ndoa Imara katika Jamii.
Dr. Ahmed Totonji (Mwenye Kanzu) akiteta Jambo na Mkurugenzi Mtendaji
wa Amana Banki Dr. Muhsin Muhsin wakati wa Kongamano la wataalamu wa Kiislam la
Kukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unaotegemewa kuanza katikati ya wiki
hii.
Mh. Asha Mtwangi akichangia Mawazo juu ya Kauli Mbiu ya Kongamano la
Kukaribisha Mwezi wa Ramadhan ambayo ilikuwa Ndoa Chanzo Cha Utu wetu ambalo
mada ya Taasisi ya Ndoa: Jana, Leo na Kesho pamoja na Familia katika Changamoto
ya utandawazi. Mh. Asha Mtwangi alihamasisha taasisi mbali mbali kuweka nguvu
zaidi kuwapa mafunzo ya dini vijana na wanandoa ili kuhakikisha wanafahamu
majukumu sahihi ndani ya ndoa.
Kwa wale ambao tulishindwa kuhudhuria kongamano hilo, tutapataje nakala za mada zilizotolewa katika kongamano hilo??
ReplyDelete