MKURUGENZI Mtendaji wa kampuni ya kuhifadhi mafuta nchini, TIPER Bw. Daniel Belair (Kulia) akikabidhi msaada wa vifaa vya maabara vyenye thamani y ash. Mil 20 kwa Afisa Mtendaji wa kata ya Bungu, wilayani Rufiji, Bw. Alli Mwamboka wakati wa hafla  fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo iliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye viwanja vya shule hiyo iliyopo wilayani Rufiji, mkoani Pwani. Msaada huo ni mwendelezo wa jitihada za kampuni hiyo katika kuisaidia jamii.

Kampuni ya kuhifadhi mafuta nchini, TIPER imetoa msaada wa vifaa vya maabara vyenye thamani ya sh. Mil. 20 kwa shule ya Sekondari Msafiri  iliyopo wilayani Rufiji, Mkoani Pwani ikiwa ni  mwendelezo wa jitihada za kampuni hiyo katika kuboresha kiwango cha elimu nchini hususani elimu ya sayansi.

Hatua hiyo imekuja miezi michache baada ya kampuni hiyo  kusaini makubaliano ya kusaidia vitabu zaidi ya 200 vya masomo ya sayansi kwa shule nyingine ya Sekondari Vijibweni iliyopo eneo la Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo iliyofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Tiper Bw. Daniel Belair alisema msaada huo pia ni sehemu ya mpango endelevu wa kampuni hiyo katika kusaidia jamii.

“Tiper tunaamini katika kuwekeza kwenye jamii inayotuzungunguka na taifa kwa ujumla hususani katika suala zima la Elimu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba uwekezaji kwenye elimu ya vijana wetu hasa kwenye sayansi ndio maandalizi ya kesho tunayoihitaji,’’ alifafanua.


Zaidi Bw.Belair alitoa wito kwa wanafunzi wa shule hiyo kuhakikisha wanavitumia kadiri iwezekanavyo vifaa hivyo sambamba na kuwa makini na utunzaji wa vifaa hivyo kwa manufaa yao na wadogo zao watakaosoma katika shule hiyo miaka ijayo.

Akizungumza pia kwenye hafla hiyo, Diwani wa kata ya Bungu Bw. Ramadhani Mkwaya alisema; “Napenda kuwashukuru Tiper kwa msaada wao huu unaolenga pia kuunga mkono mpango wa serikali wa ‘Matokeo Makubwa sasa’. Zaidi niwaombe tu wanafunzi ambao ndio walengwa wa msaada huu kuhakikisha kwamba wanawekeza zaidi kwenye masomo ya sayansi ili kuendana na mahitaji ya taifa na soko la ajira,’’.


Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo Bw. Maulid Mwita licha ya kuonyesha kufurahishwa na msaada huo aliuhakikishia uongozi wa Tiper kuwa wao kama walimu wa shule hiyo watahakikisha malengo ya kukabidhiwa vifaa hivyo yanakamilika kwa kuongeza ufahulu wa wanafunzi wao hasa kwenye masomo ya sayansi.

“Sambamba na utunzaji wa vifaa hivi, napenda kukuhakishieni kwamba ndani ya muda mfupi sana mtashuhudia ongezeko la ufahulu wa wanafunzi wetu hasa kwenye masomo ya sayansi,’’ aliahidi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kuhifadhi mafuta nchini, TIPER Bw. Daniel Belair (Kulia) akikabidhi msaada wa vifaa vya maabara vyenye thamani y ash. Mil 20 kwa Mwalimu Mkuu wa sekondari Msafiri, Bw. Maulid Mwita wakati wa hafla  fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo iliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye viwanja vya shule hiyo iliyopo wilayani Rufiji, mkoani Pwani. Msaada huo ni mwendelezo wa jitihada za kampuni hiyo katika kuisaidia jamii.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kuhifadhi mafuta nchini, TIPER Bw. Daniel Belair (Kulia) akikabidhi msaada wa vifaa vya maabara vyenye thamani y ash. Mil 20 kwa Diwani wa kata ya Bungu, wilayani Rufiji Bw.Ramadhani Makwaya  wakati wa hafla  fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo iliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye viwanja vya shule hiyo iliyopo wilayani Rufiji, mkoani Pwani. Msaada huo ni mwendelezo wa jitihada za kampuni hiyo katika kuisaidia jamii.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...