Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto) akishiriki zoezi la usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan kata ya Kivukoni ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mazingira huku akishirikiana na viongozi wa kampuni iliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd pamoja na wafanyakazi wa manispaa ya Ilala jana asubuhi. Wa pili kushoto ni Meneja wa mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena.
Mkurugenzi wa Green WastePro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo (kushoto) akifanya usafi kwenye fukwe ya Bahari ya Hindi kata ya Kivukoni karibu na maeneo ya Aga Khan sambamba na wafanyakazi wenzake pamoja na Muandaaji wa vipindi vya Orijino Komedi, Sekioni David 'Seki' (wa kwanza kulia) katika kuadhimisha wiki ya Mazingira.
Wafanyakazi wa Manispaa ya Ilala wakiendelea kufanya usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi kata ya Kivukoni eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni wiki ya Mazingira. Katikati ni Meneja wa mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2015

    Tuhifadhi mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo na vya sasa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...