Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe (aliyesimama) akizunguza wakati wa kuhitimisha kampeni dhidi ya maradhi ya Fistula katika mikoa ya kanda ya kati, mjini Dodoma jana. Waliokaa kutoka kushoto  ni Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans, Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya kati, Mruta Hamisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UNFPA, Rutasha Dadi. Kampeni hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation ilifanyika katika mikoa mitatu ikiwa na dhumuni la kutoa elimu kwa Umma na kuwasisitiza wanaume kuwaruhusu wakinamama kujitokeza ili wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.
Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya kati, Mruta Hamisi ( aliyesimama kulia) akizungumza wakati wa kuhitimisha kampeni dhidi ya maradhi ya Fistula iliyofanyika katika mikoa mitatu Nchini na kumalizikia katika mikoa ya kanda ya kati, mjini Dodoma jana.Waliokaa ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii, Dk Stephen Kebwe (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans.Kampeni hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa Umma na kuwasisitiza wanaume kuwaruhusu wakinamama kujitokeza ili wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.
Wakazi wa manispaa ya Dodoma wakihudhuria kwa wingi kwenye hitimisho la kampeni dhidi ya maradhi ya Fistula. Ambapo Naibu Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe alihitimisha kampeni hizo katika viwanja vya Mashujaa mjini Dodoma jana. Kampeni hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation ilifanyika katika mikoa mitatu ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa Umma na kuwasisitiza wanaume kuwaruhusu wakinamama kujitokeza ili wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2015

    Tatizo la fistula ni balaa kweli.
    Nafikiri ndugu wengi hawafahamu hasa tatizo hilo na inabidi kuwaelimisha ili wasiwatese na kuwanyanyasa wakina mama walio na matatizo hayo. Jambo lingine ni kwamba tatizo hilo laweza kupunguzwa kabisa kwa kuwaelimisha waja wazito na kuwaelimisha wakunga.Kuna nchi jirani kidogo nasi ambapo fistula ilikuwa balaa kubwa, na sasa wenzetu wanalipiga vita tatizo kwa kuwa na hospitali maalum ya fistula ambayo pia ni shule wa wakunga, yaani
    FISTULA HOSPITAL AND COLLEGE OF MIDWIVES

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...