Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisani moja ya fomu za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati alipofika Makao Makuu ya CCM mkoani Dodoma leo Juni 4, 2015 kwa ajili ya kuchukua fomu hizo. Kushoto ni Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni , Seif Khatib.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha mkoba wenye Fomu za kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, baada ya kukabidhiwa mkoba huo na Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni , Seif Khatib, kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CCM mkoani Dodoma leo, Juni 4, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, baada ya kuchukua fomu, leo Juni 4, 2015. Kulia ni Mzee wa Chama cha Mapinduzi, Ramadhan Suleiman Nzori.
Inawezekana kabisa mwaka 2020....wanachama wote milioni 6 wa sisiem wakatangaza nia......maana naona wajumbe wote wa mkutano mkuu wanataka urais......
ReplyDeleteHii ni nchi huru acha watangaze nia.
ReplyDelete