Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini mkataba wa makubaliano ya kuwa na soko la pamoja kwa Nchi za Wanachama wa Kanda ya tatu ya Nchi za Afrika Mashariki, Kusini mwa Afrika na za Magharibi. Dkt.Bilal pamoja na Viongozi wa Nchi husika wamesaini mkataba huo leo katika Mkutano mkuu wa tatu wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Soko la pamoja la Nchi za Kusini mwa Afrika (COMESA) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Sharm El Sheikh, nchini Misri.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Waziri wa Afrika Mashariki, Dkt. Harrison Mwakyembe, akimpongeza baada ya kusaini mkataba huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya Mawaziri wake katika mkutano mkuu wa tatu wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Soko la pamoja la Nchi za Kusini mwa Afrika (COMESA) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika leo Juni 10, 2015 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Sharm El Sheikh, nchini Misri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...