DSC_0015
Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma, Sospeter Christopher Boyo (aliyesimama mwenye shati la kitenge) akisoma taarifa fupi ya Kambi ya Nyarugusu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (aliyeketi mwenye suti ya kijivu) aliyeambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez mara baada ya kuwasili kwenye kambi hiyo kujionea hali halisi ya mazingira na changamoto zinazowakabili Waomba hifadhi wa Burundi na Kongo. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog). 
DSC_0072
Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (wa pili kushoto) akizungumza jambo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) huku Mkuu wa kambi mpya inayotarajiwa kuanzishwa ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile (wa nne kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa tatu kushoto) mara tu baada ya kuwasili na kusomewa taarifa kwenye kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Wengine pichani ni baadhi ya viongozi wa ulinzi na usalama wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
DSC_0038
Mkuu wa kambi mpya inayotarajiwa kuanzishwa ya Nyarugusu B, Fredrick Nisajile akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe wakati akitembelea na kukagua maeneo mbalimbali ya Kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
DSC_0143
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole wakikagua sehemu wanayolala Waomba hifadhi wanaoendelea kuwasili katika kambi ya Nyarugusu ambayo inaelemewa kutokana na wingi wa Waomba hifadhi hao wanaoendelea kumiminika mjini Kigoma.
DSC_0148
Muonekano wa moja ya chumba cha kulala familia za waomba hifadhi katika kambi ya Nyarugusu ambapo kifika muda wa kulala wanatandika mkeka chini katika vumbi hilo jekundu na kupata usingizi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2015

    Ukimbizi katika hali hizi ni mgumu. tuendeleze siasa safi zisizotapika wananchi katika nchi nyingine

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...