Waandishi wa habari kutoka Tanzania waliosafirishwa na Shirika la ndege lenye gharama nafuu nchini Fastjet kuhudhuria maonyesho ya Kimataifa ya Utalii ya Shanganai yanayoendelea nchini Zimbabwe. Kutoka kushoto ni Timothy Kitundu (East Africa Business Week), Mariam Said (Daily News) pamoja na Justin Damiana (The African) wakiwa wameketi kwenye mapango ya Chinhoyi huku wakibadilishana mawazo na wadau wa utalii kutoka Afrika Kusini.
Kutoka kushoto ni Victoria Siphiwe Mamvura Gava, Cherry Sibanda na Mariam Said wakiwa wamepumzika huku wakipitia baadhi ya vipeperusha vya boti za kitalii zinazokodishwa kwa ajili ya kupumzika katika ziwa la Kariba.
Kundi jingine likiwa kwenye ziara ya ziwa Kariba likiongozwa na Rumbidzai Mudzengerere wa Mamlaka ya Utalii ya Zimbabwe (ZTA).
Kituo cha mafuta katika Bandari ya Marine Land kikiwa ndani ya Ziwa Kariba. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...