Na Mwandishi wetu,Globu ya Jamii
KUONGEZEKA
kwa ndoa za utotoni inatokana na sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kuendelea
kutumika wakati hali yake ni mbaya kwa watoto wakike kushindwa kufikia ndoto zao.
Akizungumza
na katika mdahalo wa Nijali uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Regency
,Mratibu wa Utetezi Taifa ,SOS Tanzania/Zanzibar ,John Batista amesema kuongezeka kwa mimba za utotoni inatokana na
sheria ya ndoa kuendelea kutumika.
Amesema kuwa
kuendelea kwa mimba za utotoni pamoja kuolewa kunatokana sheria kutamka kuwa
mtoto anaweza kuolewa kwa miaka 14 kwa ridhaa ya wazazi.
Ripoti ya
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya Watu (UNFPA) inaonyesha
watoto 1,3822 ambao wamezaliwa katika mwaka 2005 na 2010 ifikapo 2030 watakuwa wameolewa chini
ya miaka 18.
Katika
ripoti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaonyesha wasichana 8000
wanapata ujauzito wakiwemo wanafunzi wa Shule ya msingi 3000 na ,sekondari
5000.
Mratibu wa
C-SEMA,Michael Kihongoh amesema kampeni hii ni endelevu na waandishi wametakiwa
kuweka kipaumbele kupigania sheria ya ndoa ya mtoto kuondolewa kabisa ili
watoto wa wakike waweze kulindwa.
Amesema kuwa
watoto wa kike wako katika hatari ambapo elimu inatakiwa kutolewa kwa jamii
ikiwemo malezi kwa waoto wa kike wasiweze kuingia katika vishawishi.

Mshauri
Mkuu Mwandamizi na Msimamizi wa Huduma ya Simu kwa Mtoto wa C-SEMA, Fatuma Ahmad
akizungumza na waandishi wa habari katika mdahalo wa Nijali uliofanyika katika
leo Hoteli ya Regency Jijini Dar es Salaam.
Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Watoto (TAJOC), Chalila Kibuda
akizungumza na waandishi wa habari katika mdahalo wa Nijali uliofanyika katika
leo Hoteli ya Regency Jijini Dar es Salaam.
Washiriki
wa Mdahalo wa Nijali ulioshirikisha
Chama cha Waaandishi wa habari za Watoto (TAJOC) na wadau wengine uliofanyika
leo katika Hoteli ya Regency jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...