Meneja Mradi wa Sports Development Aid (SDA) Bw.
Mohamed Chigogolo akielezea jambo wakati wa hafla ya kuwaaga watoto wanaoenda
kushiriki michuano ya Kombe la Helsinki nchini Finland, hafla hiyo imefanyika
jana katika ukumbi wa Ubalozi wa Finland jijini Dar es Salaam.Katikati ni Afisa
Michezo Mwandamizi kutoka Wizara ya Habari, Vijana, na Michezo Bw. Nicholaus
Bulamile na Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Bw. Boniface Wambura.
Balozi wa Finland nchini Bibi. Sinikka Antila
akipeana mkono wa mmoja wa wachezaji wa timu ya Vito FC ya wilayani Kilwa mkoa
wa Lindi wakati wakiagwa kwa ajili ya kuelekea nchini Finland jana jijini Dar
es Salaam. Timu hiyo inaelekea nchini humo kushiriki mashindano ya Kombe la
Helsinki ambayo yanahusisha jumla ya timu za watoto walio na umri chini ya
miaka 12.Mshindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 05 Julai 2015 na
kushirikisha zaidi ya timu 1000.
Balozi wa Finland nchini Tanzania Bibi. Sinikka
Antila akipngea na wachezaji wa Timu ya VITO FC kutoka Kilwa mkoani
Lindi, ambayo ilikuwa inaagwa kabla ya kuelekea nchini Finland kwa
ajili ya kushiriki michuano ya Kombe la Helsinki itakayoanza kutimua vumbi
tarehe 05 Julai jijini Helsinki Finland. Timu hiyo imepata ushiriki huo kupitia
Asasi ya kirai ya Sports Development Aid (SDA) ikiwa na lengo la kutumia
michezo kama nyenzo ya kuhamasisha jamii kuwapeleka watoto wao wakapate elimu.
Balozi wa Finland nchini Bibi. Sinikka Antila akiwa
katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Vito FC ya Kilwa mkoani Lindi
wakati wa hafla ya kuwaga kwa ajili ya kuelekea nchini Finland jana jijini Dar
es Salaam. Timu hiyo inaelekea nchini humo kushiriki mashindano ya Kombe la
Helsinki ambayo yanahusisha jumla ya timu za watoto walio na umri chini ya
miaka 12.Mshindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 05 Julai 2015 na
kushirikisha zaidi ya timu 1000.
Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) Bw. Boniface Wambura akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji
wa timu ya Vito FC ya Kilwa mkoani Lindi wakati wa hafla ya kuwaga kwa ajili ya
kuelekea nchini Finland jana jijini Dar es Salaam. Timu hiyo inaelekea nchini
humo kushiriki mashindano ya Kombe la Helsinki ambayo yanahusisha jumla ya timu
za watoto walio na umri chini ya miaka 12.Mshindano hayo yanatarajiwa kuanza
tarehe 05 Julai 2015 na kushirikisha zaidi ya timu 1000.
Picha na Frank Shija, WHVUM
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...