Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF - LINDI Ndg: Ramadhani Mtumwa akikabidhi Msaada wa Mifuko ya Sementi 300 kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, iliyopokelewa na Mkuu wa wilaya ya Lindi Ndg Yahaya E. Nawanda
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Ndg Yahaya E. Nawanda (Kulia) akikabidhi Msaada wa Mifuko ya Sementi 300 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Ndg Seleman Ngaweje aliyo ipokea toka kwa Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF-LINDI kwa ajili ya Umaliziaji wa Ujenzi wa Maabara katika wilaya ya Lindi Vijijini. Kaimu Mkurugenzi huyo ameshukuru mfuko huo kwani msaada huo utaweza kusaidia Umaliziaji wa Ujenzi wa Maabara katika sehemu zilizobaki katika wilaya hiyo.
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF - LINDI Ndg: Ramadhani Mtumwa akitoa maelezo juu ya Msaada wa Mifuko 300 ya Sementi iliyotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa Mkoa wa Lindi ilikumalizia ujenzi wa Maabara, Meneja huyo amesema wameweza kutoa msaada huo kwani wameguswa na suala hilo na pia kutimiza ahadi waliyompatia Mbunge wa Viti maalum kupitia CCM, Mama Lulida. Zoezi hilo la Makabidhiano Yamefanyika katika Ofisi za PSPF-LINDI
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF - LINDI Ndg: Ramadhani Mtumwa akiwa katika Picha ya Pamoja na Mkuu wa wilaya ya Lindi Ndg Yahaya E. Nawanda (mwenye suti ya kijivu) pamoja na Kaimu mkurugenzi wa wilaya ya Lindi Vijijini Ngd Selemani Gaweje, wakati wa Makabidhiano ya Mifuko 300 ya Sementi kwa ajili ya Ujenzi wa Maabara makabidhiano yaliyofanywa katika Ofisi za PSPF-LINDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...