Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Group, Bw Johnson Lukaza akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa filamu ya Mpango Mbaya iliyochezwa na washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) mwaka 2014, uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa sinema wa century uliopo Mlimani City, Jijini Dar Es Salaam. Filamu hii ni moja ya filamu ambayo ina ubora wa hali ya juu huku wadau waliofanikiwa kuitazama filamu hiyo kuvutiwa nayo na kukubali kuwa ni filamu yenye viwango vya kimataifa na yenye utofauti mkubwa na filamu nyingine za Kitanzania.
Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Group, Bw Johnson Lukaza akifurahia jambo na mwenyekiti wa bodi ya filamu nchini, Mama Fisoo kabla ya uzinduzi wa filamu ya Mpango Mbaya kuanza, uzinduzi huo ulifanyika jana katika Ukumbi wa Sinema wa Century uliopo Mlimani city, Jijini Dar Es Salaam.
Ankal Michuzi,naona hii sio kweli.Kiwango gani cha kimataifa mnazungumzia hapo? Mi naona ndio kwanza wanazidi kudidimia. Unajua hata wewe unafanya vizuri na hii blog yako kutokana na professionalism katika uandishi wa habari (hasa foto-journalism), hawa wenzetu hawaheshimu taaluma ya sanaa. Ujue filamu inaanza kwenye thieta ya jukwaani, na hivyo hapa Tanzania kwa hilo elimu ya sanaa toka Bagamoyo-TaSUBa, au FPA-Udsm haikwepeki. Angalia hilo tangazo lao katika youtube, yaani halikupi hata hamasa ya kutafuta filamu yenyewe uione. Kwanini? kwasababu kutengeneza synopsis ya trailers pia kunahitaji taaluma, na hao hawana.Uigizaji mbovu, upigaji picha ndio usiseme ni laana kuita hiyo ni filamu. Filamu ni nini? masimulizi ya hadithi katika picha zitembeazo zikisaidiwa kidogo sana na sauti. Filamu ni cinematography- sanaa ya kusimulia hadithi kwa mpangilio wa picha. Si unakumbuka tuliangalia filamu za kihindi kama "Mardi", "Hatya", "Disco Dancer", "nagni" na hata Loha bila kujua kihindi lakini filamu tuliziijoy na kuelewa kila kitu? kwanini? kwasababu cinematography ilitimia. Sasa hawa waswahili wanataka kuvuna mahindi pila palizi, mbolea hata kuvuna hivi inawezekana kweli? Ankal, mi nadhani wakati fulani tuwe wazi tuwaambie ukweli hawa jamaa zetu wa Bongo movie kuwa kuiga jinsi ya kufanya mambo na kujifunza kufanya mambo kwa kujitegemea kiujuzi na kitaaluma ni jambo la msingi. Hakuna siku filamu hizi za bongo zitafanya vizuri mpaka watakapokubali kuwa elimu ndio msingi wa yote!
ReplyDelete